10. Mja ndiye mwenye kusababisha hatma ya mafikio yake

Amewafanyia wepesi waumini kwa ambayo ni mepesi… – Amesema (Ta´ala):

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ

“Na Tutakuwepesishia kwa yaliyo mepesi.”[1]

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ

“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.[2]

Sababu ni yenye kutoka kwa mja:

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ

“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.”

Hii ni sababu yenye kutoka kwa mja:

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ

“… basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.”

Haya ni maafikisho kutoka kwa Allaah.

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ

“Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi… “

Hii ni sababu yenye kutoka kwa mja:

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ

“… basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[3]

Hii ni adhabu kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa sababu hakuikubali haki na wala hakufanya sababu ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huongoza kwazo. Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanyeni matendo! Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kuwepesishiwa kwa kile alichoumbiwa.”[4]

[1] 87:8

[2] 92:5-07

[3] 92:8-10

[4] al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 16
  • Imechapishwa: 05/07/2021