10. Mfano wa tano kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

al-Kulayniy amesema katika “al-Kaafiy”[1]:

“Mlango – hakuna yeyoye aliyeikusanya Qur-aan yote isipokuwa maamuma na wanajua kila kilichomo humo

Muhammad bin Yahyaa ameeleza kutoka kwa Ahmad bin Muhammad, kutoka kwa Mahbuub, kutoka kwa ´Amr bin Abiyl-Midqaam, kutoka kwa Jaabir ambaye amesema kuwa alimsikia Abu Ja´far akisema:

“Hakuna yeyote mwenye kusema kuwa ameikusanya Qur-aan yote kama ilivyoteremka isipokuwa atakuwa amesema uongo. Hakuna yeyote aliyeikusanya na kuihifadhi kama ilivyoteremka kwa Allaah isipokuwa ´Aliy bin Abiy Twaalib na maimamu waliokuja baada yake.””

Iko wapi Qur-aan hii ambayo hakuna yeyote aliyeikusanya isipokuwa ´Aliy bin Abiy Twaalib na maimamu waliokuja baada yake? Je, ´Aliy alipitwa na kitu ambacho maimamu baada yake wakakikamilisha? Je, kila imamu alipitwa na kitu ambacho imamu aliyekuja baada yake akakikamilisha? Tunauliza ni lini ilikamilika kukusanywa kwake? Je, imamu asiyekuwepo bado ni mwenye kushughulika na kuikusanya? Ni kwa nini maimamu wote hawa wamekubaliana juu ya kuificha kwa Ummah wa Muhammad? Je, inajuzu kwao kuificha? Je, ni wenye kusifiwa kwa kufanya hivo?

Hakuna tunachoweza kusema isipokuwa Allaah Amemtakasa Abu ´Abdillaah na maimamu na uongo huu ambao umezushwa na Raafidhwah wanafiki juu ya Kitabu cha Allaah na juu ya maimamu. Malengo yao ni kuitukana Qur-aan ya kwamba ni pungufu. Malengo yao ni kumtukana ´Aliy na kizazi chake na kuonekana kuwa ni wasaliti walioficha Kitabu cha Allaah. Hata mayahudi na manaswara hawawezi kufanya khiyana, ufichaji na ukiritimba namna hii.

[1] 01/228.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 40
  • Imechapishwa: 19/03/2017