Swali 10: Je, ni lazima tutaje mazuri ya wale tunaowatahadharisha?

Jibu: Ukitaja mazuri yao ina maana ya kwamba unaita watu wawafuate[1]. Hapana, usitaje mazuri yao. Taja makosa yao tu[2]. Huna jukumu la kupendekeza hali zao. Wewe jukumu lako ni kutaja makosa yake ili atubu kutokana nayo na ili wengine watahadhari nayo. Mazuri yao yote yanaweza kutokomea bure ikiwa makosa yao ni kufuru au shirki. Pengine vilevile yakashinda mazuri yao. Huenda yakaonekana ni mazuri kwako na yasionekane ni mazuri mbele ya Allaah.

[1] Mtu anawadanganya watu pale anapotaja mwazuri ya wazushi hata kama atataja mabaya yao. Muda  wa kuwa umemsifu watu hawatotazama makosa yake. Sio katika mfumo wa Salaf kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah wakati walipokuwa wanakosoa. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) hakumsifu Husayn al-Karaabiysiy wakati alipokuwa anabainisha hali yake. Alisema:

“Ni mzushi.”

Alitahadharisha naye na kukaa naye. Vivyo hivyo alitahadharisha kwa ukali kabisa kukaa na al-Muhaasibiy. Wakati Abu Zur´ah (Rahimahu Allaah) alipoulizwa juu ya al-Haarith al-Muhaasibiy na vitabu vyake alisema:

“Ninakutahadharisha na vitabu hivi. Vina Bid´ah na upotevu. Shikamana na mapokezi.”

Ni kitu kisichojificha kwako ya kwamba al-Karaabiysiy na al-Muhaasibiy walikuwa ni bahari ya elimu. Wao wenyewe wamewaraddi Ahl-ul-Bid´ah. Hata hivyo akasema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa na huyo mwingine akatumbukia katika kitu kama falsafa pindi alipokuwa anawaraddi wanafalsafa kwa kutumia falsafa badala ya Sunnah. Hii ndio nukta muhimu zaidi ambayo Imaam Ahmad alimkemea kwayo. (Tazama ”at-Tahdhiyb” (2/117), ”Taariykh Baghdaad” (8/215-216) na ”Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (13/110) na (12/89) ya adh-Dhahabiy.)

[2] Vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah wakati anapotaja uzushi wa watu wa Bid´ah ni dalili kubwa inayoonesha kuwa hakutajwi mazuri ya watu wa Bid´ah. Vitabu vyake vimejaa Ruduud na ukosoaji. Amewaraddi watu wa mantiki na wanafalsafa. Amewaraddi Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah. Pamoja na hivyo hatukuona akitaja kitu katika mazuri yao. Amewaraddi watu kwa kuwalenga kama vile al-Akhna´iy, al-Bakriy na wengineo pasi na kuwasifu. Bila ya shaka watu hawa wana mazuri yao, lakini hata hivyo si lazima kutaja mazuri yao wakati wa kukosoa. Zingatia hilo! Raafiy´ bin Ashras (Rahimahu Allaah) amesema:

“Miongoni mwa adhabu ya mtenda dhambi mzushi ni kutotaja mazuri yake.” (Tazama ”Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy” (1/353).)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 18/02/2017