10. Mazuri ya Ahl-ul-Bid´ah hayatajwi


Swali 10: Je, ni lazima tutaje mazuri ya wale tunaowatahadharisha?

Jibu: Ukitaja mazuri yao ina maana ya kwamba unaita watu kuwafuata[1]. Hapana, usitaje mazuri yao. Taja makosa yao tu.[2] Huna jukumu la kupendekeza hali zao. Wewe jukumu lako ni kutaja makosa yake ili atubu kwayo na ili wengine watahadhari nayo. Mazuri yao yote yanaweza kutokomea bure ikiwa makosa yao ni kufuru au shirki. Vinaweza kushinda mazuri yao. Huenda yakaonekana ni mazuri yako na mbele ya Allaah yakawa si mazuri.

[1] Hata kama mtu atataja mabaya ya watu wa Bid´ah anawadanganya watu pale atapotaja mazuri yake. Maadamu umemsifu watu hawatotazama makosa yake. Sio katika mfumo wa Salaf kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah wakati walipokuwa wanakosoa. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) hakumsifu Husayn al-Karaabiysiy wakati alipokuwa anabainisha hali yake. Alisema:

“Ni mtu wa Bid´ah.”

Alitahadharisha naye na kukaa naye. Kadhalika alitahadharisha kwa ukali kabisa kukaa na al-Muhaasibiy. Wakati Abu Zur´ah (Rahimahu Allaah) alipoulizwa juu ya al-Haarith al-Muhaasibiy na vitabu vyake alisema:

“Ninakutahadharisha na vitabu hivi. Vina Bid´ah na upotevu. Shikamana na mapokezi.”

Ni kitu unachokijua fika ya kwamba al-Karaabiysiy na al-Muhaasibiy walikuwa ni bahari ya elimu. Wao wenyewe wamewaraddi Ahl-ul-Bid´ah. Hata hivyo akasema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa na huyo mwingine akatumbukia kwenye kitu kama falsafa pindi alipokuwa anawaraddi wanafalsafa kwa kutumia falsafa badala ya Sunnah. Hii ndio nukta muhimu zaidi ambayo Imaam Ahmad alimkemea kwayo. (Tazama ”at-Tahdhiyb” (2/117), ”Taariykh Baghdaad” (8/215-216) na ”Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (13/110) na (12/89) ya adh-Dhahabiy.)

[2] Vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah wakati anapotaja uzushi wa watu wa Bid´ah ni dalili kubwa inayoonesha kuwa hakutajwi mazuri ya watu wa Bid´ah. Vitabu vyake vimejaa ruduud na ukosoaji. Amewaraddi wanamantiki na wanafalsafa. Amewaraddi Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah. Pamoja na hivyo hatukuona akitaja kitu katika sifa zao nzuri. Amewaraddi watu kama al-Akhna´iy, al-Bakriy na wengine pasina kuwasifu. Bila ya shaka watu hawa wana mazuri yao, lakini sio kitu ambacho ni lazima kukitaja wakati wa kukosoa. Zingatia hilo! Raafi´ bin Ashras (Rahimahu Allaah) amesema:

“Miongoni mwa adhabu ya mtenda dhambi mtu wa Bid´ah ni kutotaja mazuri yake.” (Tazama ”Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy” (1/353).)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 18/02/2017