Madambi yanapanda madhambi mapya na yanazalisha baadhi kwa mengine. Hali inaweza kupelekea mpaka mja akawa hawezi kuyaacha na kuyatoka. Kama walivosema baadhi ya Salaf:

“Adhabu ya dhambi ni kuwa inapelekea katika dhambi nyingine mfano wake. Thawabu za tendo jema ni kuwa inapelekea katika jema jengine mfano wake.”

Pindi mja anapotenda tendo jema, basi tendo jengine jema karibu yake linasema “Njoo na unifanye mimi pia!” Anapoitenda, lile tendo la tatu humwita na kadhalika. Kwa njia hiyo faida inakuwa kubwa zaidi na matendo mema yanazidi. Vivyo hivyo ndivyo inavyokuwa madhambi mpaka matendo mema na madhambi yanakuwa na muonekano uliokita na sifa zilizolazimiana.

Mtu mwema akiacha kutenda matendo mema, basi anahisi dhiki moyoni mwake. Anahisi kama samaki anavyokutoka ndani ya maji [kwenda nchikavu] mpaka ataporudi ndani yake. Hapo ndipo anahisi vizuri ndani ya nafsi yake.

Endapo mtenda madhambi ataacha kutenda dhambi na akaanza kufanya matendo mema, basi anahisi vibaya nafsini mwake mpaka pale ataporudi katika madhambi hayo. Kuna watenda madhambi wengi ambao wanatenda madhambi pasi na kuhisi ladha yoyote. Sababu inayomfanya kutenda dhambi ni kuwa anahisi maumivu iwapo hatendi dhambi.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 68
  • Imechapishwa: 07/01/2018