[14] Ikiwa Witr ni Rak´ah tatu, basi lililo Sunnah ni kusoma “al-A´laa” katika ile Rak´ah ya kwanza, “al-Kaafiruun” katika Rak´ah ya pili na “al-Ikhlaasw” katika Rak´ah ya tatu ambayo wakati mwingine mtu anaweza kuongeza juu yake “al-Falaq” na “an-Naas”.

Vilevile imesihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alisoma katika Witr Aayah mia moja kutoka katika “an-Nisaa´”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qiyaam Ramadhwaan, uk. 30
  • Imechapishwa: 07/05/2019