10. Kila Bid´ah ni upotevu


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Kila Bid´ah ni upotevu

Hakuna Bid´ah nzuri kama wanavyosema. Bid´ah zote ni upotevu kutokana na dalili ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Hakika kila Bid´ah ni upotevu na kila Bid´ah ni upotevu.”

Hakuna kitu kizuri katika Bid´ah hata siku moja. Bid´ah zote ni upotevu. Haya ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye hatamki kwa matamanio yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 21
  • Imechapishwa: 11/10/2017