10. Jina linafichua maumbile ya mtoto na yule mtoaji

Jina linamwelezea yule mpewaji. Ikiwa wewe unajua kitabu kinazungumzia nini pale unapotazama kichwa cha khabari yake, basi utajua pia yale mtoto anayoamini na ni maumbile gani alionayo pale utapoliona jina lake. Uhakika wa mambo ni kuwa utamuona yule aliyelichagua alivyo na upeo wa elimu yake na uoni wake.

Jina la mtoto ndio kishikilio chake chenye kumtambulisha. Mtoto amefungamanishwa na jina lake. Kupitia maana ya jina ndio mtoto hufichuka, baba yake na hali ya Ummah wake na ni tabia zipi na thamani walionayo. Pamoja na kuwa kifungamanishi kati ya jina na yule mpewaji ni chenye nguvu kabisa, jina pia linamfichua yule mpewaji. Ni jambo limekadiriwa na Yule mwenye nguvu kabisa na Mjuzi wa yote na akakiweka kwenye nafsi na mioyo ya waja. Ni nadra ukute laqabu isiyoendana na yule mwenye kuitwa nayo. Katika maneno ya watu inasemwa kuwa laqabu ni yenye kutoka mbinguni; unakaribia kutokukuta jina kali au baya isipokuwa yule aliyepewa nalo yuko hali kadhalika na kinyume chake. Katika maneno ya watu inasemwa vilevile ya kwamba kila mtu ana sehemu yake katika jina lake.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 18/03/2017