10 – Jamii kutofautiana nyoyo

Amebainisha (Ta´ala) katika Suurah “al-Hashr” kwamba suala hili sababu yake ni kutokuwa na akili. Amesema:

لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ

“Hawatopigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa kuwa katika miji iliyozatitiwa kwa ngome au nyuma ya kuta. Uadui wao baina yao ni mkali. Utawadhania wameungana pamoja kumbe nyoyo zao zimetofuatiana.”[1]

Kisha Akabainisha ni kwa nini mambo yako namna hiyo:

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ

“Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.”[2]

Ukosefu wa akili ni ugonjwa ambao dawa yake ni kufuata nuru ya Wahy. Wahy unaongoza katika manufaa ambayo hayawezi kudhibitiwa na akili:

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا

“Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo?”[3]

Hapa amebainisha kuwa nuru ya imani inamuhuisha yule ambaye ni maiti na inamwangazia njia anayopitaeko. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ

“Allaah ni kipenzi wa wale walioamini, anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru.”[4]

أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Je, yule anayekwenda akisinukia juu ya ya uso wake ni mwongofu zaidi au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka?”[5]

Kwa ufupi manufaa haya ya mwanadamu yanayojenga nidhamu za kidunia yanazunguka katika aina tatu:

Ya kwanza: Kuzuia madhara. Madhara haya kwa wanachuoni yanajulikana kama ´mambo ya kidharurah`. Yanahusiana na kuzuia madhara katika nyanja sita tulizozitaja kabla:

1 – Dini.

2 – Nafsi.

3 – Akili.

4 – Nasaba.

5 – Heshima.

6 – Mali.

Ya pili: Kuleta na kufikia manufaa. Manufaa haya kwa wanachuoni yanajulikana kama ´mahitaji´. Katika matawi yake ni biashara na deni kwa mujibu wa maoni yanayoonelea hivo. Kadhalika inahusiana na manufaa mengine yote ya kubadilishana baina ya watu katika jamii kwa njia ya Kishari´ah.

Ya tatu: Kujipamba kwa tabia na desturi nzuri. Katika vitaga vyake ni zile sifa za kimaumbile kama kuziachia ndevu, kuyapunguza masharubu, uchafu wa haramu na kuwapa matumizi ndugu mafukara.

Hakuna yeyote wala chochote kinachohifadhi manufaa haya kwa njia ya hekima na nzuri zaidi kama Uislamu:

الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ

“Alif Laam Raa. Hiki ni Kitabu ambacho Aayah Zake zimetimizwa barabara kisha zikapambanuliwa vyema kutoka kwa Aliye na hekima na Mwenye khabari zote za ndani na za nje.”[6]

Swalah na amani zimwendee Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] 59:14

[2] 59:14

[3] 06:122

[4] 02:257

[5] 67:22

[6] 11:01

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 14/06/2023