10. Hadiyth “Kuna ambao Allaah huwaacha huru kila kunapofunguliwa swawm… “


1001- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuna ambao Allaah huwaacha huru kila kunapofunguliwa swawm.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi usiokuwa na neno, at-Twabaraaniy na al-Bayhaqiy ambaye amesema:

“Hadiyth hii ni geni kwa vile mkubwa amesimulia kutoka kwa mdogo. Naye si mwengine ni al-A´mash ambaye amesimulia kutoka kwa al-Husayn bin Waaqid.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/586)
  • Imechapishwa: 26/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy