10. Hadiyth “Akitawadha mja ambapo akasukutua kinywa… “

185 – ´Abdullaah bin as-Sunaabihiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Akitawadha mja ambapo akasukutua kinywa, basi yanaondoka makosa yake kinywani mwake. Akipenga, basi yanaondoka makosa puani mwake. Akiosha uso wake, basi yanaondoka makosa usoni mwake mpaka yanatoka chini ya kope zake. Akiosha mikono yake, basi yanaondoka makosa yake mikononi mwake mpaka yanatoka chini ya kucha za mikono yake. Akifuta kichwa chake kwa mikono yake, basi yanaondoka makosa yake kichwa mwake mpaka yanatoka masikioni mwake. Akiosha miguu yake, basi yanaondoka makosa miguuni mwake mpaka yanatoka chini ya kucha za miguu yake. Kisha kule kutembea kwake kwenda msikitini na swalah yake inakuwa ni ziada ya thawabu.”[1]

Ameipokea Maalik, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na al-Haakim ambaye amesema:

“Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Haina kasoro. as-Sunaabihiy alikuwa ni Swahabah anayetambulika.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/191)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy