10. Fadhilah ya pili ya funga: Allaah ndiye anailipa


2- Allaah amesema kuhusu swawm:

“… na mimi Ndiye nitailipa.”

Ameegemeza malipo kwa nafsi Yake tukufu. Kwa sababu matendo mema zinaongezwa thawabu zake kwa idadi ya jema moja kwa kumi na mfano wake mpaka mara mia saba na zaidi ya hapo. Kuhusiana na funga Allaah ameegemeza malipo kwa nafsi Yake pasi na kuzingatia idadi – Naye (Subhaanah) ndiye mkarimu zaidi wa wenye kukirimu, mtoaji sana katika wenye kutoa. Zawadi zinakuwa kwa kiasi cha yule mtoaji. Kwa hivyo ujira wa swawm unakuwa mkubwa zaidi na mwingi pasi na hesabu.

Swawm ni kusubiri juu ya kumtii Allaah, kusubiri juu ya yale Allaah aliyoharamisha, kusubiri juu ya makadirio ya Allaah kutokana na njaa, kiu, kunyongeka kwa mwili na nafsi. Juu yake kumekusanyika aina tatu za subira na imehakikika kweli kuwa mfungaji ni miongoni mwa wenye kusubiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Hakika wale wenye kusubiri watalipwa kikamilifu ujira wao pasi na hesabu.”[1]

[1] 39:10

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 08/04/2020