10. Fadhila za kidini zilizoko Shaam

Shaam ni ardhi ya Jihaad. Wakazi wake wanaishi katika Jihaad na ulinzi wa mipaka ya utawala wa Kiislamu. Matumizi yao kwao wenyewe ni kama matumizi katika njia ya Allaah; yanalipwa mara mia saba.

74- Abud-Dardaa’ alimwandikia Salmaan:

“Njoo katika ardhi Takatifu! Ardhi ya Jihaad!”

75- Kwa ajili hiyo Salaf walikuwa wakichagua kuishi Shaam kwa ajili tu ya Jihaad. Kwa mfano hivyo ndivyo walivyofanya waislamu kutoka Quraysh walioingia katika Uislamu wakati wa kutekwa kwa Makkah.

76- Artwa´ah bin al-Mundhir ameeleza kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu walio na ujira mkubwa ni mwanamme mdogo Shaam ambaye kachukua kamba wa farasi wake. Anaiangalia migongo ya waislamu na hajui kama mnyamamkali atamvamia au adui akamghushi.”

77- Ibn ´Uyaynah na wanachuoni wengine walikuwa wakisema:

“Anayetaka elimu ya vita basi ashikamane na watu wa Shaam. Kutokana na wingi wa Jihaad yao ndio wajuzi zaidi juu ya hukumu za Jihaad.”

78- ash-Shaafi´iy amesema:

“Anayetaka elimu ya vita basi ashikamane na watu wa Shaam.”

79- Sa´iyd bin Sufyaan al-Qaariy amesema:

“Ndugu yangu alifariki na akaacha ameusia dinari mia moja katika njia ya Allaah. Mwaka huo hakukukuwa Jihaad. Nikafika al-Madiynah wakati wa hajj au ´umrah. Nikaingia ndani kwa ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh). Kwake kulikuwepo mwanamme aliyekaa. Nikasema: “Ee kiongozi wa waumini! Ndugu yangu amefariki na ameacha anausia dinari mia moja katika njia ya Allaah. Hatukuwa na vita yoyote. Unaniamuru nifanye nini?” ´Uthmaan akasema: “Allaah ametuamrisha kuwa waislamu na tukasilimu. Sote ni waislamu. Halafu akatuamrisha kuhajiri tukahajiri kwenda al-Madiynah. Sisi ni wahajiri wa al-Madiynah. Kisha akatuamrisha kutoka kwenda katika Jihaad na mkawa mmetoka kwenda katika Jihaad. Nyiyni ni mujahidina wa Shaam. Zitumie juu ya nafsi yako, familia yako na wale wahitaji waliyoko pembezoni mwako. Ukinunua nyama kwa dirhamu moja na ukala wewe pamoja na familia yako basi unaandikiwa dirhamu mia saba.” Nikatoka na nikauliza juu ya yule mwanaume aliyekuwa amekaa kwake. Alikuwa ni ´Aliy bin Abiy Twaalib.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 90-92
  • Imechapishwa: 10/02/2017