10. Du´aa ya kuingia nyumbani na wakati wa kula


46- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi mtu anapoingia nyumbani na akamtaja Allaah (Ta´ala) wakati anapoingia na wakati wa kula Shaytwaan husema: “Hamna pa kulala wala chakula.” Akiingia pasina kumtaja Allaah (Ta´ala) Shaytwaan husema: “Mmepata pa kulala.” Na ikiwa hakumtaja Allaah (Ta´ala) wakati wa kula husema: “Mmepata pa kulala na chakula.”

47- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ewe mwanangu! Unapoingia (nyumbani) kwa ahli zako toa Salaam. Inakuwa ni baraka kwako na kwa familia yako.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 21/03/2017