Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… akaturuzuku…

MAELEZO

Dalili ya jambo hili ni nyingi katika Qur-aan, Sunnah na akili. Ama kuhusu Qur-aan, Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

“Hakika Allaah ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu kali madhubuti.” (adh-Dhaariyaat 51 : 58)

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُلِ اللَّـهُ

“Sema: “Nani yule anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini?”  Sema: “Ni Allaah!” (Sabaa´ 34 : 24)

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ

“Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini au nani anayemiliki kusikia na kuona na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu na anayemtoa mfu kutoka aliye uhai na nani anayeendesha mambo yote?   Watasema: “Ni Allaah.” (Yuunus 10 : 31)

Kuhusu Sunnah ni pamoja na yale aliyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba kuna Malaika anayetumwa kwa kwa kipomoko na anaamrishwa kuandika mambo mane; riziki yake, muda wake wa kuishi, matendo yake na kama atakuwa mwenye furaha na mla khasara.

Kuhusiana na dalili ya kiakili juu ya kwamba Allaah ameturuzuku ni kwa sababu hatuwezi kuishi pas na chakula na kinywaji ambavyo vimeumbwa na Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema:

أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ إِنَّا لَمُغْرَمُونَ بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ

”Je, mnaona mimea mnayopanda? Je, ni nyinyi ndio mlioiotesha au Sisi ndio tulioiotesha? Lau Tungelitaka basi tungeliifanya haizai, mkabakia   mnanung’unika; [huku mkisema:] “Hakika sisi tumegharimika! Bali sisi tumenyimwa!” Je, mnaona maji ambayo mnakunywa? Je, ni nyinyi ndio mliyoyateremsha mawinguni au Sisi ndio wateremshaji? Lau Tungelitaka basi tungeliyafanya machungu basi kwa nini hamshukuru?” (al-Waaqi´ah 56 : 63-70)

Katika Aayah hizi kumebainishwa ya kwamba chakula chetu na kinywaji kinatokana na Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 18/05/2020