10. Cha kwanza mchumbiaji huangalia huwa ni uso


Miongoni mwa dalili za Sunnah ni:

1- Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mmoja wenu akimchumbia mwanamke hakuna neno akamwangalia pasina yeye kujua ikiwa kama anamwangalia ili amchumbie.”[1]

Ameipokea Ahmad. al-Haythamiy amesema katika “Majma´-uz-Zawaa´id”:

“Wanaume wake ni wanaume Swahiyh.”

Kinacholengwa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa sio dhambi kwa mchumbiaji peke yake kumwangalia yule anayefikiria kumuoa ikiwa malengo ni kutaka kumchumbia. Ni dalili inayoonesha kuwa ni haramu kwa hali yoyote kwa yule asiyefikiria kuchumbia. Hali kadhalika ikiwa mchumbiaji hana nia ya kuchumbia isipokuwa anamwangalia kwa sababu tu ya kutaka kuburudika na mfano wa hayo.

Huenda mtu akasema Hadiyth haikuweka wazi ni kipi cha kuangalia; inawezekana ikawa ni kifua na matiti. Pamoja na hivyo kila mtu ni mwenye kujua kwamba anacholenga mchumbiaji ni uzuri wa uso. Aghlabu vinginevyo huwa si lengo. Mchumbiaji hutazama uso. Ni jambo lisilokuwa na shaka mwenye kutaka uzuri anacholenga huwa ni uso.

[1] Ahmad (24000).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 26/03/2017