10. Asiyewakufurisha washirikina hakukufuru Twaaghuut

Asiyekuwakufurisha washirikina ina maana ya kwamba hakukufuru Twaaghuut. Kwa msemo mwingine ni kwamba amekubali shirki. Mwenye kutilia shaka juu ya ukafiri wa mayahudi na manaswara au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi hakukufuru Twaaghuut. Hivyo basi hawi muumini. Kwa hiyo dalili juu ya kwamba asiyewakufurisha washirikina, akatilia shaka ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi ni kalima ya Tawhiyd “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” kwa sababu hakukufuru Twaaghuut. Vilevile Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

“Basi atakayemkanusha twaaghuut [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti.”[1]

Kama tulivyotangulia kusema ya kwamba Tawhiyd na imani havipatikani isipokuwa kwa mambo mawili; kukufuru Twaaghuut na kumuamini Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana kalima ya Tawhiyd ambayo ni “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” ndani yake mna ukanushaji na uthibitishaji.

[1] 02:256

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 10/04/2023