10. al-Halabiy anajitolea ushahidi kwa Muhammad al-Imaam

al-Halabiy amesema:

“Mambo mengi ambayo Shaykh al-Halabiy ameyaweka katika kitabu chake yanaafikiana na yaliyo kwenye kitabu cha Shaykh Muhammad al-Imaam katika kitabu chake “al-Ibaanah”.”[1]

Hata hivyo Shaykh al-Imaam alikosea wakati alipokubaliana na misingi ya al-Halabiy. Kutolea dalili kwa makosa ya wengine ni jambo lenye kuonesha kuwa umezama katika matamanio. Ni wanachuoni wepi wa Salafiyyuun waliyokupendekeza wewe na kupendekeza kitabu chako kilichoandikwa ili kupiga vita mfumo wa Salaf? Kukosekana kwa mapendekezo yao si ni dalili ya wazi yenye kuonyesha ubatili na kwenda kinyume na mfumo wa Salaf?

[1] Uk. 1

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017