Allaah (Ta´ala) amesema:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ

“Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan… “[1]

Katika kipande hichi inapata kutubainikia kuwa Qur-aan imeteremshwa katika Ramadhaan. Ni katika usiku gani iliteremka? Usiku wa Makadirio. Hili linatufanya kuamini kwa kukata kabisa ya kwamba usiku wa Makadirio uko katika Ramadhaan. Wako wanaosema kuwa usiku wa Makadirio unaweza kuwa katika Ramadhaan na nje ya Ramadhaan. Hata hivyo ni vigumu kulenga unakuwa katika usiku gani. Maoni yaliyo karibu na usawa ni kwamba unakuwa katika yale masiku kumi ya mwisho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utafuteni katika yale masiku kumi ya mwisho Ramadhaan na utafuteni katika kila usiku wa witiri.”

Usiku wa witiri ni usiku wa tarehe 21, 23, 25, 27 na 29 Ramadhaan.

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametusahilishia kwa kutujuza ya kwamba ameiteremsha Qur-aan katika Ramadhaan. Katika Aayah nyingine amesema (Ta´ala):

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ

“Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-aan katika usiku wa Makadirio.”[2]

 Hiyo haimaanishi kwamba ndipo ilipoteremka yote. Aayah hii inaweza kuwa na maana mbili:

1- Inaweza kuwa inalenga kwamba ndipo Qur-aan ilipoanza kuteremka kwa mara ya kwanza. Ilianza kuteremka katika usiku huo na ikaendelea kuteremka kwa miaka ishirini na tatu mpaka pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofariki.

2- Inaweza kuwa inalenga kwamba ndipo ilipoteremshwa katika nyumba yenye Nguvu kwa mara moja, kama alivyosema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Kisha ikawa inateremshwa hatua kwa hatua.

[1] 02:185

[2] 97:01

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 19-22
  • Imechapishwa: 02/06/2017