Ndani yake mna milango:

Mlango wa kwanza: Vitangulizi vya funga. Ndani yake mna masuala yafuatayo:

Suala la kwanza: Utambulizo wa swawm na ubainifu wa nguzo zake.

1- Utambulisho wake: Maana ya funga kilugha ni kujizuia kutokamana na kitu.

Maana yake katika Shari´ah ni kujizuia kutokamana na kula, kunywa na vifunguzi vyengine pamoja na nia. Kuanzia pale ambapo kunaingia alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa jua.

2- Nguzo zake: Kupitia utambulisho wa funga kwa mujibu wa dini imepata kubainika kwamba inazo nguzo mbili za kimsingi:

Ya kwanza: Kujizuia na vifunguzi kuanzia pale ambapo kunachomoza alfajiri mpaka kuzama kwa jua. Dalili ya nguzo hii ni maneno Yake (Ta´ala):

فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Basi sasa waingilieni na tafuteni yale aliyokuandikieni Allaah kwenu. Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi Kisha timizeni funga mpaka usiku.”[1]

Makusudio ya nyuzi nyeupe na nyusi nyeusi ni kubaini kwa mchana na giza la usiku.

Ya pili: Mfungaji akusudie kwa kujizuia huku kutokamana vifunguzi kumwabudu Allaah (´Azza wa Jall). Kwa nia ndio kunabaini matendo ambayo yamekusudiwa ´ibaadah na matendo mengine. Kwa ndio kunapambanuka ´ibaadah kutokamana na zengine. Hivyo mfungaji anakusudia kwa funga hii ima funga ya Ramadhaan au aina nyingine ya swawm katika zile zilizopendekezwa. Dalili ya nguzo hii ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika matendo yote yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”[2]

[1] 02:187

[2] al-Bukhaariy (01) na Muslim (1907).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 149
  • Imechapishwa: 13/04/2020