1. Mfano wa kwanza kuonyesha kuwa Raafidhwah ni Baatwiniyyah

Nitataja baadhi ya mifano kuonyesha kuwa Raafidhwah ni Baatwiniyyah:

1- al-´Ayyaashiy (01/42) amesema:

“Jaabir al-Ju´fiy ameeleza kuwa alimuuliza Abu Ja´far kuhusu tafsiri iliyojificha juu ya Aayah:

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ

“Na aminini yale Niliyoyateremsha [hivi sasa] yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi [mliyoteremshiwa] na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha.” (02:41)

Akasema:

“Maana yake ni fulani na wenzake na wale wote wenye kufuata dini yao. Hawa ndio Allaah Anaowakusudia wakati Anaposema:

وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ

“… na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha.”

Mhakiki ameelekeza katika “al-Bihaar”, “al-Burhaan” na Ithbaat-ul-Hudaah”.

Allaah Amemtakasa Abu Ja´far na tafsiri hii ya ki-Baatwiniy ambapo Baatwiniyyah wanakusudia kumkufurisha Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Wanaozungumzishwa katika Aayah hii, na ilio kabla yake, inawaelekea wanaisraeli ambapo Allaah Anawaamrisha kuiamini Qur-aan ambayo Allaah Ameiteremsha ikisadikisha yale waliyopata, nayo ni Tawrat ambayo Allaah Aliiteremsha kwa Mtume Wake Muusa, na Anawakataza kuikanusha Qur-aan hii tukufu inayosadikisha yale waliyomo. Hivyo basi, Baatwiniyyah wameyapotosha Maneno ya Allaah khatari kuliko mayahudi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 29
  • Imechapishwa: 18/03/2017