Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye, kumtaka msaada na msamaha. Tunajilinde Kwake kutokana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule anayeongozwa na Allaah, basi hakuna awezae kumpoteza, na yule anayepotezwa na Allaah, basi hakuna awezae kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Amma ba´d:

Kijitabu chetu cha leo ni chenye kuthibitisha ya kwamba Swalah ya ´Iyd Sunnah ni kuiswali katika uwanja wa kuswalia (مصلى) nje ya mji. Nilikuwa nimefikiria kukifanya kijitabu cha jumla kilichokusanya hukumu za Swalah ya ´Iyd kama jinsi nilivyofanya na “Swalaat-ut-Taraawiyh”. Lakini kwa vile muda umekuwa mfinyu – kunabaki siku chache ´Iyd-ul-Fitwr ifike – nimedharurika kukifupisha. Hata hivyo ninataraji kuwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atanisahilishia kukitoa kwa muda mfupi na kueneza kitabu kilicho cha jumla kitachoenezwa kwa watu. Kadhalika ninamuomba Allaah atukubalie kijitabu chetu kwa njia nzuri na pia waniombee katika du´aa zao za siri huenda – Allaah akitaka – akaninufaisha:

يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ

“Siku ambayo hayatofaa mali wa watoto. Isipokuwa yule atakayefika kwa Allaah na moyo uliosalimika.”[1]

[1] 26:88-89

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swalâat-ul-´Iydayn, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 11/05/2020