1- Maendeleo ya kwanza ya al-Ikhwaan al-Muslimuun


Allaah ndiye lengo letu, Mtume ndio kiongozi wetu na Qur-aan ndio katiba yetu.

Huu ndio msingi wao ambao wameijaza dunia mpaka hii leo. Kwa uinje unaonekana ni wa sawa na wazi. Allaah ndiye mjuzi zaidi wa yaliyomo kwenye mioyo na yale wanayoficha. Tazama hivi sasa jinsi msingi huu umevobadilika kwenye maendeleo matatu ambayo yanaenda kinyume kabisa na msingi wenyewe.

Msingi wa kwanza:

Kiongozi wa jumla (Hasan al-Bannaa) aliweka wazi kwenye gazeti “al-Muswawwar” lililotoka siku ya ijumaa tarehe 05 aprili 1946. Meritt Beg Ghali na Shaykh Louis Fanous ni wanachama wa al-Ikhwaan al-Muslimuun na wanawafanyia kazi. Tungelipendelea al-Ikhwaan al-Muslimuun wangeliwasaidia wagombea wa Louis Fanous kwenye ubunge kutokamana na kwamba ni mmoja katika wanachama wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Hivyo tumeelekeza kwenye maneno ya kiongozi wa jumla Hasan al-Bannaa ambaye aliandika ifuatavyo:

“Kamati ya al-Ikhwaan al-Muslimuun ina marafiki wengi wasiokuwa waislamu. al-Ikhwaan al-Muslimuun inawazingatia wote kama marafiki. Ni wanachama wanaofanya kazi kwenye nyanja zote za kijamii ambapo wanastahiki. Wanawaacha waweze kunufaisha kwa maoni na fikira zao.

Ndugu na profesa Nassif Michael alishiriki na kuandaa mkutano wa al-Ikhwaan al-Muslimuun huko al-Gharbiyyah kwa kiasi cha kwamba sintokuwa mwenye kupetuka mipaka lau nitasema kuwa yeye ndio aliandaa mkutano mzima.

Sintosahau pia ndugu na muheshimiwaji Shaykh Louis Fanous safari zake kwa ajili ya mikutano ya al-Ikhwaan al-Muslimuun na propaganda zote anazofanya za mikusanyiko katika Misri.

Hali kadhalika ndugu Meritt Beg Ghali alishiriki kwenye kazi za al-Ikhwaan al-Muslimuun. Sintosahau pia msaada wake wa kifedha wa jengo na msaada wa kifasihi kwa aina ya kubadilisha fikira na mawazo kwenye ustawi wa kijamii, seuze ya kwamba ni mwanachama kwenye uongozi wetu wa kiuchumi. Vilevile alishirikiana na sisi kwenye miradi ya kijamii na yenye manufaa.

Nimeyataja majina haya tu kama mfano. Hatuoni kizuizi chochote kabisa cha kushirikiana na raia wafanya kazi, manaswara kwa waislamu. Hili linaweka wazi kabisa ya kwamba washirika wa al-Ikhwaan wana watu thelathini kutoka kwa ndugu zetu manaswara.

Kuhusiana na uchaguzi, kanuni yetu ni kuanza kuwasaidia wagombea wa al-Ikhwaan. Hawawachagui isipokuwa watu wa Misri tu walio na busara. Wakati al-Ikhwaan wanapowaweka hadharani wagombea wao kwa ajili ya uchaguzi basi watu wote watajua kuwa sisi hatuwazingatii isipokuwa tu wale wenye ustawi wa jumla. Katika majina watawapata ndugu zetu manaswara ambao wanashirikiana na sisi kwenye mikutano.

Baada ya wagombea wa al-Ikhwaan tunawasaidia vilevile wale wagombea wenye uwezo zaidi wa kuweza kutumikia ustawi wa jamii kwa jumla pasina kuangalia kama ana dini nyingine au chama kingine maadamu inahusiana na maslahi ya Misri na watu wa Misri.”

 

Waandishi: Shaykh Ahmad Shaakir, Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Afiyfiy, Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Wakiyl, Shaykh Muhammad Khaliyl al-Harraas, Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy na wengineo.
Marejeo: Gazeti al-Hadiy an-Nabawiy (1365/6)
Mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy
Chanzo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 7-9