Himdi zote anastahiki Allaah. Swalah na salaam zimwendee Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na wenye kufuata uongofu wao:

Amma ba´d:

´Aliy al-Halabiy ana mielekeo mingi ikiwa ni pamoja na:

1- Kupetuka kwake mipaka kwa kupenda uongozi. Anafanya kila aliwezalo ili aweze kuufikia

2. Kupetuka kwake mipaka kwa kupenda mali. Anafanya kila aliwezalo kwa kuweza kuzipata.

Amewauzia Dini yake maadui wa mfumo wa Salaf na Salafiyyuun. Anaingia ndani ya Kauli Yake (Ta´ala):

اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا عَن سَبِيلِهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Wamenunua ujumbe wa Allaah kwa thamani ndogo na wakazuilia [watu] njia Yake [Allaah]. Hakika ni mabaya waliyokuwa wakitenda.” (09:9)

Mapenzi yake ya kupenda uongozi na mali yamemfanya kujiunga na kila mwenye kueneza fitina na kushambulia mfumo wa Salaf na Salafiyyuun.

Ana mfumo mpana. Anapatana na watu wote wenye mifumo inayoenda kinyume. Ni ndugu wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Ni ndugu wa Qutbiyyuun na Takfiyriyyuun. Ni ndugu wa wale wanaolingania katika umoja wa dini na uhuru wa dini. Ni ndugu wa kila mwenye kutetea madhehebu haya na wafuasi wake. Kwa mujibu wake wote hawa wamesalimika na upetukaji mipaka. Kwa mujibu wake wapetukaji mipaka ni Salafiyyuun tu kwa sababu wanapambana na mielekeo hii ya batili na watu wake kwa mizani ya Kiislamu isiyokubaliana na mfumo uliomkubwa na mpana wa al-Halabiy unaopatia nafasi mifumo yote hii inayoenda kinyume. Ndio maana anaonelea kuwa ni lazima kupambana na mfumo wa Salaf na Salafiyyuun. Anawaita kuwa ni wapetukaji mipaka na anawapachika jina hili wao. Si yeye wala pote lake hawabadili msimamo huu. Hawauachi na wala hawajatosheka nao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017