Imesuniwa kumkumbusha mgonjwa kuacha anausia na kutubia?

Swali: Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa imesuniwa kumkumbusha mgonjwa kufanya tawbah na kuusia na kuna wanaosema kuwa hili linahusiana na yale maradhi ya khatari na si yale maradhi mepesi. Ni yapi maoni yako?

Jibu: Naonelea kuwa inatakiwa kumkumbusha mgonjwa kufanya tawbah na kuusia. Tawbah na kuusia ni mambo yamewekwa katika Shari´ah wakati wowote ule. Lakini mtu afanye hivo kwa njia isiyomshtua mgonjwa1.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/71)
  • Imechapishwa: 17/06/2017