1. Haki ya Allaah juu ya waja na haki ya waja kwa Allaah


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.” (ad-Dhaariyaat 51: 52)

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

2- “Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.”(an-Nahl 16 : 32)

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا

3- ”Na Mola wako Ameamrisha ya kwamba, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye Pekee. Na [amekuamrisheni] kuwatendea wema wazazi wawili.” (al-Israa´ 17 : 23-24)

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

4- “Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe Yeye na chochote.” (an-Nisaa´ 04:36)

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖوَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَوَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

5- ”Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu kwamba: Msimshirikishe na chochote; na muwafanyie wema wazazi wawili; na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini – Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao – na wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri na yaliyo siri; na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kutia akilini. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia bora [ya kumtengenezea hicho chake] mpaka afikie kubalege. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu – Hatukalifishi nafsi isipokuwa vile inavyoweza. – Na mnaposema [katika kushuhudia] basi semeni kwa uadilifu, japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah.” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kukumbuka. Allaah anasema: “Hii ndio njia Yangu, [njia] iliyonyooka; basi ifuateni na wala msifuate njia [nyinginezo] vitakufarikisheni na njia Yake!” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na kucha.” (al-An´aam 06 : 151-153)

6- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule anayetaka kuona wasia wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Mtume ameweka muhuri wake, basi asome Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖوَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَوَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَوَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

”Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu kwamba: Msimshirikishe na chochote; na muwafanyie wema wazazi wawili; na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini – Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao – na wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri na yaliyo siri; na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kutia akilini. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia bora [ya kumtengenezea hicho chake] mpaka afikie kubalege. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu – Hatukalifishi nafsi isipokuwa vile inavyoweza. – Na mnaposema [katika kushuhudia] basi semeni kwa uadilifu, japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah.” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kukumbuka. Allaah anasema: “Hii ndio njia Yangu, [njia] iliyonyooka; basi ifuateni na wala msifuate njia [nyinginezo] vitakufarikisheni na njia Yake!” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na kucha.”[1] (al-An´aam 06 : 151-153)

7- Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya punda. Akanambia: “Ee Mu´aadh! Je, unajua ni ipi haki ya Allaah juu waja na haki ya waja kwa Allaah?” Nikasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: “Haki ya Allaah juu ya waja wamuabudu Yeye na wala wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kutomuadhibu yule ambaye hakumshirikisha Yeye na chochote.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nisiwabashirie watu?” Akasema: “Usiwabashirie wakaja kutegemea hivyo.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

1- Maana ya Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah na ´ibaadah.

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.” (adh-Dhaariyaat 51: 52)

Hii ndio hekima ya Kishari´ah ya wao kuumbwa. Allaah hakuwaumba ili waje kuongeza idadi. Amewaumba ili awape majaribio. Alalah (Ta´ala) amesema:

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ

“Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Naye ni Mwenye  nguvu kabisa, Mwingi wa kusamehe.” (al-Mulk 67 : 02)

لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا

“Ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi Wake.” (atw-Twalaaq 65 : 12)

Allaah amewaumba ili awafunze kuwa Yeye ndio Muumbaji, Mrukuzakaji na Muwezaji. Allaah amewapa majaribio kwa maamrisho, makatazo na majukumu ili waweze kumuabudu kwa ujuzi. Kwa ajili hiyo ndio maana amewatuma Mitume na akateremsha Vitabu ili aweze kujifunza haki Yake na washikamane nayo:

2- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.”(an-Nahl 16 : 32)

Bi maana muabuduni Allaah pekee na jiepusheni na Twaaghuut. Twaghuut ni kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah na huku kimeridhia hilo. Kuhusiana na wale wenye kuabudiwa badala ya Allaah pasi kuridhia hilo, kama Mitume na Manabii, sio Twaahuut. Kwa sababu wao hawakuamrishah ilo.

3- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا

”Na Mola wako Ameamrisha ya kwamba, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye Pekee. Na [amekuamrisheni] kuwatendea wema wazazi wawili.” (al-Israa´ 17 : 23-24)

Bi maana amekuamrisheni na kukuusieni kumuabudu Allaah Pekee. Yeye ndiye ambaye anastahiki ´ibaadah. Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Hii ina maana ya kwamba hakuna zaidi ya Allaah ambaye ana haki ya kuabudiwa. Hivyo basi muabudu Yeye peke yake na wala usimshirikishe Yeye katika ´ibaadah Zake na chochote sawa ikiwa ni Mtume, Malaika, walii au mtu mwingine. Ni juu ya mtu kutahadhari na aina zote za shirki.

4-

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

 “Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe Yeye na chochote.”(an-Nisaa´ 04:36)

5-

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖوَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَوَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

”Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu kwamba: Msimshirikishe na chochote; na muwafanyie wema wazazi wawili; na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini – Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao – na wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri na yaliyo siri; na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kutia akilini. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia bora [ya kumtengenezea hicho chake] mpaka afikie kubalege. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu – Hatukalifishi nafsi isipokuwa vile inavyoweza. – Na mnaposema [katika kushuhudia] basi semeni kwa uadilifu, japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah.” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni [Allaah] kwayo mpate kukumbuka. Allaah anasema: “Hii ndio njia Yangu, [njia] iliyonyooka; basi ifuateni na wala msifuate njia [nyinginezo] vitakufarikisheni na njia Yake!” Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na kucha.” (al-An´aam 06 : 151-153)

Allaah anamwamrisha Mtume kuwaeleza watu yale aliyoharamisha na awasomee kwa elimu na yakini na sio kwa shaka na dhana. Jambo la kwanza katika mambo haya yaliyoharamishwa ni shirki. Allaah ameharamisha shirki kama ambavyo vilevile ameharamisha mambo ya haramu mengine yote. La kwanza katika mambo ya haramu yote haya ni shirki. Shirki maana yake ni kufanya aina yoyote ile ya ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah. Aayah hizi zimebeba mambo kumi:

La kwanza: Shirki.

La pili: Kuwatendea wema wazazi wawili. Kutajwa kwao baada ya Allaah kunatolea dalili kuonesha ukubwa wa haki zao. Kuwatunza vibaya wazazi wawili ni moja katika madhambi makubwa. Allaah ametaja haki zao sambamba pamoja na haki Yake katika Aayah nyingi.

La tatu: Kutowaua watoto.

La nne: Kutoyakaribia machafu kama usengenyaji, uvumi, uzinifu na wizi.

La tano: Kutoiua nafsi yoyote iliyoharamishwa na Allaah kuia pasi na haki.

La sita: Kutokula mali ya yatima. Yatima ni yule ambaye amefisha baba yake kabla ya kubaleghe.

La saba: Kutimiza kipimo na mizani.

La nane: Kutimiza ahadi ya Allaah. Ahadi ya Allaah ni ´ibaadah aliyoamrisha na apwekeshwe katika ´ibaadah na kuepuka makatazo Yake.

La tisa: Ahadi.

Wasia ni maamrisho yenye kukaziwa. Mtu anausia jambo pale anapolikokoteza. Wenye busara ni wale wenye kuyafahamu mambo haya na wakashikamana nayo kwa akili zao.

Allaah amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ

“Hii ndio njia Yangu, [njia] iliyonyooka; basi ifuateni… ”

Njia ya Allaah ni kutekeleza maamrisho Yake, kujiepusha na makatazo Yake na kumtakasia Yeye katika ´ibaadah. Ni wajibu kwa watu kushikamana bara bara na njia hii. Allaah (Ta´ala) amesema:

 

وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ

“… na wala msifuate njia [nyinginezo].”

Njia nyinginezo ni Bid´ah, matamanio na shahawa za haramu. Allaah ameanza kutaja akili kwa sababu mwanaadamu huanza kufikiri kwanza. Kisha anatafakari, anajifunza na kukumbuka. Halafu baada ya hapo ndio anaogopa na kufanya yale yenye kumnufaisha na kujiepusha na yale yenye kumdhuru na kumkasirikisha Mola Wake.

6- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule anayetaka kuona wasia wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Mtume ameweka muhuri wake, basi asome… “

Bi maana ni kana kwamba aliandika na kupiga saini yake. Huu ndio wasia wa Allaah na wasia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah walihuzunishwa pindi walipomuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anataka kuacha anausia. Hatimaye akawa ameacha kufanya hivo. Alipotaka kuacha anausia baadhi yao walionelea aletewe karatasi na wengine wakaonelea asisumbuliwe kwa vile anaumwa. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamrisha watoke na kusema:

“Haitakiwi walumbane kwangu.”

Ibn ´Abbaas amesema:

“Ni ajali kubwa kuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuacha anaandika wasia.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, si mnipe kiapo cha usikivu na utiifu kwa Aayah hizi?”[3]

7- Mu´aadh bin Jaba (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya punda.. “

Katika Hadiyth hii kunaonesha unyenyekevu wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tabia nzuri aliokuwa nayo kwa njia mbali mbali. Kwa mfano kupanda kwake juu ya punda, kuwa na mtu mwingine nyuma yake ambaye anazungumza naye tofauti na wanavofanya baadhi ya watu waliokuwa na kiburi.

Katika Hadiyth hii kunaonesha pia jinsi faida na hukumu zinavyotolewa kupitia kwa njia ya maswali. Hili hushika kwenye mioyo ya wasikilizaji. Vilevile ni jambo linalomuandaa na kumpa moyo wa kujibu swali msikilizaji. Tofauti na lau mada itaanza kutajwa moja kwa moja. Kuna khatari ya mtu kutoizingatia.

Mu´aadh bin Jabal amesema:

“Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.”

Kuna tabia nzuri ya Mu´aadh ambapo hakujikakama kwa kitu asichokijua. Ikiwa mtu hawezi kujibu swali ni wajibu kwake kusema “Sijui” au “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi” ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuhai. Baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu anatakiwa kusema “Allaah ndio anajua zaidi” au “Sijui”. Asisemi “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi” kwa vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui yale waliyoyafanya watu baada ya kufa kwake. Katika Hadiyth ya Hodhi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Maswahabah zangu! Maswahabah zangu!” Ndipo ataambiwa: “Hakika wewe hujui waliyoyafanya baada yako.”[4]

[1] al-Bukhaariy (2856) na Muslim (30)

[2] at-Tirmidhiy (3070), al-Bayhaqiy katika ”Shu´ab-ul-Iymaan” (7918) na at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” (1186). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaany katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy”.

[3] al-Haakim (3240) na al-Marwaziy katika ”Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah” (2/615).

[4] al-Bukhaariy (4625) na Muslim (2860).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 11-14
  • Imechapishwa: 10/04/2015