1. Dibaji ya “Fusuwl fiys-Swiyaam wat-Taraawiyh waz-Zakaah”

Himdi zote ni za Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumwomba msaada na msamaha. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na shari ya nafsi zetu na matendo yetu maovu. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule anayepotezwa na Allaah, hakuna wa kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirikina, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja na Mtume Wake. Swalah na salaam zimwendee yeye, ahli zake, Maswahabah zake na yule mwenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

Amma ba´d:

Kwa mnasaba wa kuja kwa mwezi wa Ramadhaan uliyobarikiwa ninawawasilishia ndugu zetu waislamu sura ifuatayo. Ninamuomba Allaah (Ta´ala) ajaalie kazi hii iwe imefanywa kwa ajili Yake, iwe ni yenye kuafikiana na Shari´ah Yake na iwanufaishe waja Wake. Hakika Yeye ni mwingi wa kutoa na ni Mkarimu.

Sura ya kwanza: Hukumu ya swawm

Sura ya pili: Hekima ya swawm na faida zake

Sura ya tatu: Swawm ya mgonjwa na msafiri

Sura ya nne: Mambo yenye kuvunja swawm

Sura ya tano: Tarawiyh

Sura ya sita: Zakaah na faida zake

Sura ya saba: Wanaostahiki kupewa zakaah

Sura ya tisa: Zakaat-ul-Fitwr

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fusuwl fiys-Swiyaam wat-Taraawiyh waz-Zakaah, uk. 2
  • Imechapishwa: 03/06/2017