1. Dibaji ya “al-Irhaab”


Himdi zote zinamstahikia Allaah zenye kutosheleza. Swalah na salaam ziwe juu ya waja na Mitume wake watukufu na wale wabwana wapwekeshaji kutoka katika kizazi cha Muhammad; wale waliopenda kwa ajili ya Allaah, wenye huruma, wenye hekima, wakweli, waliozitimiza ahadi zao. Amma ba´d:

Baada ya kufikiria na kuchunguza yanayoendelea hii leo ulimwenguni kote ambayo ni fitina za vikundivikundi (Hizbiyyah) na harakati za kigaidi katika nchi nyingi za Kiislamu, ndipo nikapendelea kuandika kazi fupi inayohusiana na mambo ya kigaidi na yale matokeo yake mabaya kwa watu katika Ummah na jamii, usalama wake na imani yake. Mambo haya ya kigaidi ni matunda ya ule ugaidi wa kifikira uliyosheheni kwenye vitabu, vipeperushi na mikanda ya wanaharakati katika kisiwa cha Kiarabu na katika miji mingine. Malengo ya kazi hii ni kuinusuru haki na kuiweka wazi njia iliyonyooka ili wale wenye kutaka waweze kuipita na upande mwingine wale wakaidi hoja iwasimamie – na Allaah ndiye mjuzi wa nia zote.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 9
  • Imechapishwa: 31/03/2017