09. Umuhimu wa jina analopewa mtoto


Jina la mtoto ndio lenye kumtambulisha na kumtofautisha kwa njia inayolingana na utukufu wake kwa aina ya kuwa ni muislamu. Ndio maana wanachuoni wameafikiana juu ya kwamba ni lazima mtoto kuwa na jina[1]. Pasi na jina mtoto anakuwa si mwenye kujulikana na mwenye kuchanganya na wengine. Jina linamtia kikomo mtoto na kumtambulisha.

Tazama jinsi Muhaddithuun wanavyofanya wanapotazama mlolongo wa wapokezi na kuona jina la mtu mwenye kutatiza; wanaifanya kuwa ni dhaifu mpaka jina lile lijulikane.

Baba akienda kinyume na uhalisia huu na akaacha kumchagulia mtoto jina linaloafikiana na Shari´ah na lugha ya kiarabu, basi uchaguzi huu utasababisha magomvi kati ya utukufu wa mtoto kama mtu wa Kiislamu na uchaguzi mbaya. Kwa hivyo hapa tunapata kuona umuhimu wa jina na ni kwa nini ni katika mambo yenye kupewa kipaumbele.

Jina ndio kitu cha kwanza mtoto hupewa pindi anapozaliwa.

Jina ndio kitu cha kwanza mtoto hujitofautisha na wengine.

Jina ndio kitu cha kwanza baba humpa mtoto, kitu chenye kuashiria urithi na uendeleaji.

Jina ndio ngazi ya kwanza mtoto huchukua ili atambulike katika jamii.

Haya yanaonesha umuhimu wa jina.

[1] Maraatib-ul-Ijmaa´, uk. 154, ya Ibn Hazm.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 18/03/2017