09. Ufafanuzi wa kwanza wa Kitaab-ut-Tawhiyd


Allaah amenufaisha kwa kitabu hiki. Wanafunzi wakawa ni wenye kukihifadhi, wanachuoni wakikisherehesha na kukiweka wazi. Mtu wa kwanza kukisherehesha ni mjukuu wa mtunzi wa kitabu ambaye ni Shaykh Sulaymaan bin ´Abdillaah. Ufafanuzi huo unaitwa “Taysiyr-ul-´Aziyz al-Hamiyd”. Lakini hata hivyo mwandishi wa kitabu (Rahimahu Allaah) alikufa kabla ya kukimaliza.

Baadaye akaja mjukuu mwengine wa Shaykh ambaye alikifupisha na akamaliza ule ufafanuzi wa kwanza. Anaitwa Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hasan na kitabu kinaitwa “Fath-ul-Majiyd”.

Kisha ufafanuzi huo ulifupishwa na idadi ya vitabu kadhaa kukiwemo:

1 – Shaykh Hamad bin ´Atiyq. Kitabu kinaitwa ”Ibtwaal-ut-Tandiyd”.

2 – Maelezo ya chini ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Qaasim.

3 – Sulaymaan bin Hamdaan.

Kitabu kina fafanuzi zengine, za zamani na za sasa. Vipo vitabu vyengine vya kazi za vyuovikuu juu ya kitabu hicho. Tunamuomba Allaah aendelee kunufaisha vizazi vinavyokuja kupitia kitabu hiki kama alivyonufaisha vizazi vilivyotangulia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 10/09/2019