09. Udhaifu mkubwa kwa watu wa Fiqh-ul-Waaqiy´ – sababu kubwa ya kujivugumiza katika yasiyokuwa fani yao

Pindi tulipozukiwa na watu hawa wenye mirengo mipya ndipo wakaifanyia elimu jinai na matendo. Ndio maana unyonge katika elimu na matendo ni kitu kinachoonekana wazi kwa vijana wa Ummah. Utawaona vijana wa Fiqh-ul-Waaqiy´ hawashikamani na hukumu nyingi za dini katika mambo mengi makubwamakubwa.

Kwa hiyo ni lazima kwa vijana wetu kumcha Allaah juu ya nafsi zao. Wanatakiwa kuzishughulisha nafsi zao juu ya yale mambo ambayo faida yake kubwa itawarudilia wao katika dini na dunia yao. Ama kujishughulisha na mambo yasiyokuwa na faida na mtu akaivugumiza nafsi yake ndani ya mambo yasiyokuwa fani yake, basi jambo hilo majanga yake ni makubwa na mtu anapitwa na kiasi kikubwa cha ujira na kheri.

Kwa hivyo vijana wanatakiwa kumcha Allaah juu ya nafsi zao na wafanyie kazi yale waliyojifunza katika elimu mpaka wafaulu dini na dunia.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 35
  • Imechapishwa: 05/08/2020