09. Sunnah kumswalia Mtume, na si maulidi

Kuhusu kumswalia na kumtakia amani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni miongoni mwa ´ibaadah na matendo bora. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Hivyo enyi walioamini mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayeniswalia mara moja, basi Allaah atamsifu mara kumi.”[2]

Ni jambo limewekwa katika Shari´ah katika nyakati zote na limesisitizwa mwishoni mwa kila swalah. Bali ni jambo la lazima kwa mujibu wa kikosi cha wanazuoni katika Tashahhud ya mwisho katika kila swalah na ni Sunnah iliokokotezwa maeneo mengi kukiwemo baada ya adhaana, wakati anapotajwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), siku ya ijumaa na usiku wake. Hayo yamejulishwa na Hadiyth nyingi.

[1] 33:56

[2] Muslim (384).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 12/01/2022