Swali 09: Ni yepi maoni yako juu ya wale walioruhusiwa kuacha kufunga kama mfano wa mzee mtumzima na mgonjwa ambaye maradhi yake hayatarajiwi kupona – je, inawalazimu kutoa fidia kutokana na kule kuacha kwao kufunga?

Jibu: Ni lazima kwa yule asiyeweza kufunga kutokana na utuuzima au ugonjwa usiotarajiwa kupona anatakiwa kulisha masikini kwa kila siku moja atakayoacha akiwa na uwezo wa kufanya hivo. Hivi ndivo walivyojibu kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) akiwemo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 18/04/2019