09. Mwenye maradhi ya moyo anaweza kuacha kufunga?

Swali 09: Inajuzu kwa mwenye maradhi ya moyo kuacha kufunga?

Jibu: Maradhi ya moyo yanatofautiana. Ikiwa maradhi ya moyo ni mepesi na yanakuja muda kwa mwingine, ni wajibu kufunga. Ni wajibu vilevile kuyaepuka yale mambo yanayozidisha maradhi. Ikiwa maradhi ya moyo ni mazito kwa njia ya kwamba haiwezekani kufunga au kunayazidisha maradhi, anatakiwa aache kuufunga na badala yake alishe kwa kila siku moja masikini. Akipona baada ya hapo anatakiwa kulipa masiku yaliyobaki. Ikiwa maradhi hayatarajiwi kupona hakuna kingine kinachomlazimu zaidi ya hicho.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 12/06/2017