09. Mtu katika maisha yake ana khiyari

Inabaini ya kwamba mwanaadamu anafanya matendo yake ya khiyari kwa kutaka na sio kwa kulazimishwa. Kama anavyotenda matendo katika dunia hii kwa khiyari na anachagua bidhaa fulani kwa mapenzi yake kadhalika anapita njia yake ya kumweleza Aakhirah kwa khiyari. Uhakika wa mambo ni kwamba njia inayoelekeza Aakhirah iko wazi zaidi kuliko njia ya dunia hii. Kwa kuwa njia ya kwenda Aakhirah imebainishwa na Allaah (Ta´ala) katika Qur-aan na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo ni lazima njia ya kwenda Aakhirah iwe bainifu na wazi zaidi. Pamoja na hivyo mwanaadamu anachukua njia ya dunia hii ambayo haimdhaminishi matunda yake na anaiacha njia ya kwenda Aakhirah ambayo matunda yake ni yenye kudhaminiwa na ni yenye kujulikana kwa kuwa Allaah ameyathibitisha – na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) havunji ahadi Yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/222)
  • Imechapishwa: 25/10/2016