09. Mke mwema hatakiwi kukufuru neema kwa mume wake

Katika sifa za mke mwema ni kwamba si mwenye kukufuru neema anazopewa. Kwa msemo mwingine ni  kwamba hakufuru neema ambazo Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) amemfanyia wepesi kupitia mume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyewashukuru watu hamshukuru Allaah.”[1]

al-Bukhaariy amepokea katika “al-Adab al-Mufrad”[2] kupitia kwa Asmaa´ bint Yaziyd al-Answaariyyah ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinipitia wakati nilikuwa nimesimama na kundi la wanawake la rika langu. Akatusalimia na kusema: “Tahadharini na kukufuru neema.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nini maana ya kukufuru neema?” Akasema: “Huenda mmoja wenu ndoa yake ikaakhirishwa kisha baadaye Allaah Akamruzuku mume na akazaa naye watoto. Wakati anapokuwa ni mwenye kukasirika siku moja anakufuru
na kusema: “Sijawahi kamwe kuona kheri yoyote
kutoka kwako.”

an-Nasaa´iy amepokea katika “as-Sunan” al-Kubraa”[3] kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Amr ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah Hamtazami mwanamke ambaye hamshukuru mume wake wakati huohuo hawezi kujitosheleza naye [kukosa
kuwa pamoja naye].”

[1] Ahmad (7939) na Abu Daawuud (4811) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh). Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swhaiyh katika ”as-Swahiyhah” (416).

[2] 1048. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (823).

[3] 9135. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (289).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 04/08/2018