09. Mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika kumwabudu Allaah


2- Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika kumwabudu Allaah:

Mfumo wao ni kwamba wanamwabudu kwa ajili ya Allaah, kwa jina la Allaah na kwa Allaah.

Kusema kwamba wanamwabudu Allaah kwa ajili ya Allaah hiyo ina maana ya kuwa wanamtakasia nia Allaah (´Azza wa Jall). Hawakusudii jengine kwa ´ibaadah zao isipokuwa Mola wao. Hawajikurubishi kwa mwengine asiyekuwa Yeye. Hakika wao:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza na wanataraji rehema Zake na wanakhofu adhabu Yake.”[1]

Hawamwabudu Allaah kwa sababu fulani anawaona. Hawamwabudu Allaah kwa sababu wakwazike mbele ya watu. Hawamwabudu Allaah kwa sababu wanaitwa ´waja`. Wanamwabudu Allaah kwa ajili Yake.

Kusema kwamba wanamwabudu Allaah kwa jina Lake maana yake ni kwamba ni wenye kufanya hivo kwa kumtaka msaada Yeye. Hawawezi kujifakhari nafsi zao au wakaona kuwa ni wenye kujitosheleza kutokamana na Allaah katika kuabudu kwao. Bali wao ni wenye kuhakiki maneno ya Allaah (Ta´ala):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”[2]

Maneno Yake (Ta´ala):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu.”

Bi maana wanaabudu kwa ajili ya Allaah.

Maneno Yake (Ta´ala):

وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”

Bi maana wanaabudu kwa jina la Allaah. Wanamtaka msaada katika kumwabudu kwao (Tabaarak wa Ta´ala).

Kusema kwamba wanamwabudu Allaah kwa Allaah maana yake ni katika dini ya Allaah ambayo ameiweka kupitia Mitume Wake. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika Ummah huu wanamwabudu Allaah kwa yale waliyowekewa Shari´ah kupitia Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawaongezi wala kupunguza juu yake. Wanamwabudu Allaah kwa Allaah bi maana kwa mujibu wa Shari´ah Yake na hawatoki ndani yake. Ni mamoja kwa kuongeza au kwa kupunguza. Kwa ajili hiyo ´ibaadah yao ikawa ya haki na iliosalimika kutokamana na uchafu wa shirki na Bid´ah. Kwa sababu yule mwenye kumkusudia mwengine asiyekuwa Allaah katika ´ibaadah yake basi ameshirikisha na yule mwenye kumwabudu Allaah kinyume na Shari´ah Yake amezua katika dini Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini kwa imani safi kabisa na ya asli na wasimamishe swalah na watoe zakah – na hiyo ndiyo dini iliyosimama sawasawa.”[3]

Kumwabudu kwao Allaah katika dini Yake hawazui yale ambayo matamanio yao yanayaona kuwa ni mazuri. Sisemi yale ambayo akili zao imeyaona kuwa ni mazuri. Kwa sababu akili iliosalimika haiyaoni kuwa ni mazuri yale yanayotoka nje ya Shari´ah ya Allaah. Kwa sababu akili iliosalimika inapelekea kulazimiana na Shariah ya Allaah. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alikuwa akiwakataza wale amabo wanamkadhibisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutumia akili zao na akisema:

بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ

“Bali wengi wao hawaelewi.”[4]

Lau tungelikuwa tunamwabudu Allaah kwa yale yanayotamaniwa na nafsi zetu na kwa mujibu wa matamanio yetu basi tungelikuwa makundi-makundi. Ingekuwa kila mmoja anakiona kizuri kile anachokitaka na kuanzia hapo anaanza kumwabudu nacho Allaah. Hapo isingelihakikika kwetu sifa ya Allaah pale aliposema:

وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً

“Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja.”[5]

[1] 17:57

[2] 01:05

[3] 85:05

[4] 29:63

[5] 23:52

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 11/07/2019