Bid´ah ni zile ´ibaadah, I´tiqaad au maneno yasiyokuwa na dalili katika Qur-aan na Sunnah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo dmri yetu itarudishwa.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Atakayezusha katika amri yetu hii yasiyokuwemo yatarudishwa.”[2]

“Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[3]

Bid´ah ni yale yaliyozushwa katika dini ilihali hayamo. Vipi tutajua kuwa hayamo? Hayana dalili. Lisilokuwa na dalili basi si katika dini. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu.” (05:03)

Dini imekamilika. Dini mambo ya kuzidisha. Hakuna juu yetu isipokuwa kujua dini aliyotukamilishia Allaah (´Azza wa Jall) ili tushikamana nayo na kuacha mambo ya ziada, yenye kuonekana kuwa ni mazuri na ya nyongeza. Mambo haya yanamtenga mtu mbali na Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim (1718).

[2] al-Bukhaariy (2550) na Muslim (1718).

[3] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 20
  • Imechapishwa: 11/10/2017