09. Kutawadha kati ya vitendo viwili vya ndoa

7- Kutawadha kati ya vitendo viwili vya ndoa

Akimwingilia ile sehemu inayokubalika Kishari´ah kisha akataka kumrudilia, basi anatakiwa kutawadha kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atapomwingilia mmoja mkewe kisha akataka kumrudilia basi atawadhe [kati yake wudhuu´].”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Atapomwingilia mmoja mkewe kisha akataka kumrudilia basi atawadhe wudhuu´ wa swalah, [kwani kufanya hivo kuna uchangamfu wa kurudi].”[1]

[1] Ameipokea Muslim (01/171), Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (02/51/1), Ahmad (03/28), Abu Nu´aym katika “at-Twib” (01/12/02) na nyongeza ni yake na wasiokuwa wao kupiti Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy. Nimeipokea katika “Swahiyh Sunna Abiy Daawuud” kwa nambari. 216.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 107
  • Imechapishwa: 08/03/2018