09. Kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah


Swali 9: Je, kuna ubaya wowote kutahadharisha mapote haya yanayoenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Sisi tunatahadharisha kila mwenye kwenda kinyume kwa jumla[1] na tunasema kuwa tunashikamana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuacha kila chenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hatujali sawa uhalifu ikiwa ni mkubwa au mdogo. Kwa sababu tukichukulia usahali wa uhalifu kuna khatari ukawa mkubwa. Uhalifu haujuzu kwa hali yoyote ile. Lililo la wajibu ni kufuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika mamdo makubwa na madogo.

[1] Namna hii ndivyo walivokuwa Salaf. Hawakuwa wakinyamaza. Waliwakemea wenye kunyamaza. Muhammad bin Bandaar al-Jurjaaniy alimwambia Imaam Ahmad: “Mimi kwangu naona ugumu kusema fulani yuko kadhaa na kadhaa.” Ahmad akasema: “Wewe ukinyamaza na mimi nikanyamaza – ni lini mjinga atajua lililo la salama na lililo na ugonjwa?” (Tazama ” ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231) na ”Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy” (1/350).)

Wakati Imaam Ahmad walipoulizwa kuhusu Husayn al-Karaabiysiy alisema:

“Ni mtu wa Bid´ah.”

Amesema sehemu nyingine:

“Ninakutahadharisha na Husayn al-Karaabiysiy! Usizungumze naye! Usizungumze na yule mwenye kuzungumza naye!”

Alisema hivo mara nne au tano. (Tazama “Taariykh Baghdaad” (08/65).)

Salaf walikuwa wanaonelea kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni bora kuliko kufunga, kuswali na kukaa I´tikaaf. Imaam Ahmad aliulizwa linalopendekezwa kwake ni mtu afunge, aswali, akae I´tikaaf au atahadharishe Ahl-ul-Bid´ah. Akasema:

“Akifunga, akiswali na kufanya I´tikaaf ni jambo lenye manufaa kwake tu. Lakini akitahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni jambo lenye manufaa kwa waislamu.” (Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231).)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 18/02/2017