09. Khatari ya kumzulia muumini


Jambo la saba mimi namkumbusha daktari Hadiyth iliyopokelewa na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Mwenye kumzulia uongo muumini mwanaume au muumini mwanamke basi Allaah atamzuilia mahala pa uchafu wa watu wa Motoni mpaka ayaache aliyoyasema – na hatoweza kufanya hivo.”[1]

al-Qurtwuubiy ametaja matamshi yafuatayo pasi na marejeo:

“Mwenye kumzulia uongo muumini mwanaume au muumini mwanamke basi Allaah atamzuilia mahala pa uchafu wa watu wa Motoni mpaka ayaache aliyoyasema.”

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (13469) na ”al-Mu´jam al-Awsatw” (6491). al-Haythamiy amesema:

“Wapokezi wake ndio wapokezi sahihi zaidi  isipokuwa Muhammad bin Mansuur at-Twuusiy ambaye ni mwaminifu.”(Majma´-uz-Zawaa-id (10/91).

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (437).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 11/11/2018