09. Kasumba za madhehebu zilivyopelekea kugawanyika waislamu

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Mambo yakawa amri ya kuwa na umoja katika dini hasemi jambo hilo isipokuwa zindiki au mwendawazimu.

MAELEZO

Ambaye anaamrisha kuwa na umoja na kuacha kuwa na tofauti wanasema kuwa huyu ametoka nje ya ummah na kwamba ni zindiki kwa sababu anapuuza maneno ya wanazuoni. Sisi hatupuuzi maneno ya wanazuoni. Tunachofanya ni kuyalinganisha na Kitabu cha Allaah. Hatukufaradhishiwa kuwafuata watu. Tulichoamrishwa ni kufuata Qur-aan na Sunnah. Hii ndio haki. Hatukuamrishwa kumfuata fulani na fulani. Allaah (Ta´ala) hakututegemeza juu ya maoni na Ijtihaad zetu. Kinyume chake ametuteremshia Qur-aan na akatutumia Mtume Wake. Lau tutarejea katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi migogoro na tofauti zitatoweka na kutapatikana umoja.

Mnajua kuwa si zamani sana katika msikiti Mtakatifu wa Makkah kulikuwa Mihraab nne. Kila dhehebu linaswali swalah ya mkusanyiko yao pamoja na watu wa madhehebu yake pembezoni mwa Ka´bah. Hali iliendelea hivo mpaka hapo Allaah alipofanya kupatikane mtu ambaye aliwakusanya wote kuswali nyuma ya imamu mmoja na muonekano huu mbaya ukawa umeisha na himdi zote njema anastahiki Allaah. Yote haya sababu yake ni kufuata mambo ya madhehebu na maoni. Walitofautiana mpaka katika swalah na ikawa Hanafiy haswali nyuma ya Hanbaliy na Hanbaliy haswali nyuma ya Shaafi´iy! Isitoshe jengine ni kwamba hawaswali katika wakati mmoja ambapo wamoja wanaswali mwanzoni mwa wakati na wengine wanaswali mwishoni mwa wakati! Kwa sababu fulani anaonelea lililo la sawa ni kuchelewesha swalah na mwingine anaonelea sawa ni kuitanguliza. Wanachotaka ni kuwaridhisha watu wote! Mambo haya tumeyaona katika baadhi ya miji mingine mpaka hii leo yapo. Swalah ya ijumaa hawaiswali katika wakati mmoja. Baadhi yao wanaiswali wakati wa ´Aswr kwa sababu tu fulani amesema kadhaa na kadhaa. Mmoja wao akitaka kuswali mapema wanaenda na kuswali pamoja na fulani na mwingine akitaka kuchelewesha swalah wanaenda na kuswali pamoja na fulani. Lakini hapa kwetu – himdi zote njema ni za Allaah – katika nchi hii na chini ya kivuli cha Da´wah hii iliyobarikiwa wamerudi katika yale waliyokuwemo Salaf ambapo wanaswali pamoja na kwa wakati mmoja na nyuma ya imamu mmoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 18/05/2021