5- Mfungaji kutoa damu kwa kufanya chuku ni jambo linaharibu na kumfunguza mfungaji. Haya ndio maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Haya ni kutokana na yale aliyopokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi wake kupitia kwa Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mtu al-Baqiy´ siku ya kumi na nane ya Ramadhaan na huku akifanya chuku akaushika mkono wangu na akasema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”

Kumepokelewa kuhusiana na haya kutoka kwa kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)[2].

Kundi la wanachuoni, kama mfano wa Ahmad bin Hanbal, Ishaaq bin Raahuyah na Abu Thawr, wamechagua maoni yanayosema kuwa kupiga chuku kunamfunguza yule mwenye kufunga. Vilevile hayo ndio maoni ya ´Atwaa´, ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, al-Awzaa´iy, al-Hasan na Ibn Siyriyn. Hayo ndio maoni wanayoona wafuasi wa Imaam ash-Shaafi´iy. Hili pia ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn-ul-Qayyim (Rahimahuma Allaah).

Jamhuri ya wanachuoni wameona kuwa kufanya chuku hakufunguzi kabisa. Haya ni maoni ya Maalik, ash-Shaafi´iy, Abu Haniyfah na baadhi ya Maswahabah na Taabi´uun.

[1][1] Abu Daawuud (2367) na Ibn Maajah (1680).

[2] Tazama ”Tahdhiyb-us-Sunan” (04/511).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 18/04/2019