1  – Imaam an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´” kuhusu kupaka hina:

“Kuhusu kupaka hina mikononi na miguuni ni jambo limependekezwa kwa wanawake walioolewa kutokana na Hadiyth zilizotangaa juu yake.”[1]

Anaashiria yale yaliyopokelewa na Abu Daawuud ya kwamba kuna mwanamke alimuuliza ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kuhusu upakaji hina ambapo akajibu:

“Hakuna neno. Lakini hata hivyo mimi nalichukia. Hakika mpenzi wangu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichukia harufu yake.”

Ameipokea an-Nasaa´iy.

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mwanamke mmoja alimuashiria Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyuma ya pazia kitabu ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakamata mkono wake na akasema: “Sijui ni mkono wa mwanaume au mkono wa mwanamke?” Akasema: “Ni mkono wa mwanamke.” Akasema: “Ungelikuwa ni mwanamke basi ungelibadilisha [rangi] kucha zako.”

Bi maana kuzibadilisha kwa hina.

Ameipokea Abu Daawuud na an-Nasaa´iy.

Lakini asipake rangi kucha zake kwa rangi ambayo inamganda na kuzuia twahara yake.

[1] (01/324).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 23/10/2019