Sunnah ilio na umuhimu katika uweka Shari´ah ni ile iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia za kielimu, milolongo ya wapokezi Swahiyh inayotambulika kwa wanachuoni wa Hadiyth na wapokezi wake. Sio zile Hadiyth zilizomo katika vitabu mbalimbali vya tafsiri ya Qur-aan, Fiqh, vya kuvutia na vya kutia khofu, vya kuzigonga nyoyo, vya mawaidha na vinginevyo. Hakika ndani ya vitabu hivyo kuna Hadiyth nyingi ambazo ni dhaifu, zenye kukataliwa, zilizotungwa na nyenginezo ambazo Uislamu hauna lolote nazo. Mfano wa Hadiyth hizo ni ile ya Haaruut na Maaruut, kisa kinachozungumzia kuwa al-Gharaaniyq ni walii. Kuna kijitabu maalum kinachobatilisha kisa hiki[1] na tayari kimeshachapishwa. Nimeorodhesha sehemu kubwa ya Hadiyth hizo katika kitabu kikubwa kinachoitwa “Silsilah Ahaadiyth-id-Dhwa´iyfah wal-Mawdhwu´ah wa atharuhaa as-Sayyi-a fiyl-Ummah”. Mpaka sasa Hadiyth hizo zimefikia idadi ya karibu elfu nne. Hadiyth hizo ni kati ya zilizo dhaifu na zilizotungwa. Mpaka sasa kumeshachapishwa mia tano peke yake.

[1] Kinaitwa ”Naswb al-Majaaniyq fiy nifsw qiswat-ul-Gharaaniyq”. Chapa ya “Maktabat-ul-Islaamiy”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 10/02/2017