09. Hadiyth “Tulikuwa tukisafiri pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… “


Hadiyth ya pili

2- Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Tulikuwa tukisafiri pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yule mwenye kufunga hakumkosoa yule ambaye hakufunga na yule ambaye hakufunga hakumkosoa yule ambaye amefunga.”

Maana ya kijumla:

Maswahabah walikuwa wakisafiri pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo baadhi yao wanakula na baadhi ya wengine wanafunga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakubalia juu ya hilo. Kwa sababu kufunga ndio msingi na kula ni ruhusa. Hakuna makemeo ya kuacha kutendea kazi ruhusa. Kwa ajili hiyo ndio maana baadhi hawakuwakosoa wengine juu ya kufunga au kuacha kufunga.

Faida zinazochukuliwa kutoka katika Hadiyth:

1- Inafaa kuacha kufunga safarini.

2- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakubalia Maswahabah wake juu ya kufunga na kuacha kufunga safarini. Ni dalili inayofahamisha kwamba yote mawili yameruhusiwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Bassaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-´Allaam Sharh ´Umdat-il-Ahkaam, uk. (01/326)
  • Imechapishwa: 04/06/2018