732- Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Alisimama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa ni Khatwiyb siku ya ijumaa akasema: “Pengine mtu ikamfikia ijumaa akiwa kiasi cha mili moja [mbali na mji] kisha asihudhurie.” Halafu akasema mara ya pili: “Pengine mtu ikamfikia ijumaa akiwa kiasi cha maili mbili [mbali na mji] kisha asihudhurie.” Akasema mara ya tatu: “Pengine mtu ikamfikia ijumaa akiwa kiasi cha maili tatu [mbali na mji] kisha asihudhurie ambapo Allaah akaupiga muhuri moyo wake.”[1]

Ameipokea Abu Ya´laa kwa cheni ya wapokezi ambayo ni laini[2]. Ibn Maajah amepokea kutoka kwake kwa cheni ya wapokezi ambayo ni nzuri:

“Yule mwenye kuacha ijumaa mara tatu pasi na dharurah, basi Allaah atapiga muhuri juu ya moyo wake.”[3]

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Hadiyth hii ni nzuri kutokana na Hadiyth ya kabla yake na pia kutokana na Hadiyth ya Jaabir ilio baada yake.

[3] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/452-453)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy