09. Hadiyth “Mwezi huu umekufikieni… “


100- Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati Ramadhaan ilipoingia:

“Mwezi huu umekufikieni. Ndani yamo mna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Mwenye kunyimwa kheri zake basi kwa kweli amenyimwa kheri zote. Hakuna mwenye kunyimwa kheri zake isipokuwa yule aliyenyimwa kikweli.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa mlolongo wa wapokezi mzuri – Allaah akitaka.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/586)
  • Imechapishwa: 26/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy