184 – Amesimulia tena:

“Aliomba maji ambapo akatawadha kisha akaanza kucheka. Akawaambia wenzie: “Hamniulizi ni kipi kimenichekesha?” Wakasema: “Ni kipi chenye kukuchekesha, ee kiongozi wa waumini?” Akasema: “Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha kama nilivyotawadha kisha akaanza kucheka na akasema: “Hamniulizi ni kipi kimenichekesha?” Wakasema: “Ni kipi chenye kukuchekesha, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Mja akiomba maji ya kutawadha ambapo akaosha uso wake, basi Allaah huondosha makosa yote aliyofanya kwa uso wake. Akiosha mikono yake basi inakuwa vivyo hivyo, na akisafisha miguu yake inakuwa vivyo hivyo.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri na Abu Ya´laa. al-Bazzaar ameipokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh na amezidisha juu yake:

“Na akifuta kichwa chake basi inakuwa vivyo hivyo.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/191)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy