09. Hadiyth “Lazimiana na swawm…. “


986- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilisema: “Ee Mtume wa Allaah! Niamrishe kitendo.” Akasema: “Lazimiana na swawm. Hakuna badala yake.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Niamrishe kitendo.” Akasema: “Lazimiana na swawm. Hakuna badala yake.”[1]

Ameipokea an-Nasaa´iy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake, namna hii na bila ya kukariri. Vilevile kwa al-Haakim (ambaye ameisahihisha) na kwa an-Nasaa´iy imekuja:

“Nilimjia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Niamrishe amri ambayo Allaah ataninufaisha kwayo.” Akasema: “Lazimiana na swawm. Hakuna badala yake.”[2]

Katika “as-Swahiyh” ya Ibn Hibbaan imekuja:

“Nilisema: “Ee Mtume wa Allaah! Nielekeze kwenye kitendo ambacho nitaingia Peponi kwacho.” Akasema: “Lazimiana na swawm. Hakuna mfano wake.”

Mida ya mchana kulikuwa hakuonekani moshi kwa Abu Umaamah isipokuwa anapofikiwa na wageni.[3]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

[3] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/580)
  • Imechapishwa: 29/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy